Frequently Asked Questions

Chuo chetu kipo Kizimbani Zanzibar nje kidogo ya mji wa Zanzibar, unaweza kupata fomu zetu kwa kuja moja kwa moja au kupitia tovuti yetu mara tu matangazo ya masomo yatakapotoka kwa muhula mpya.

Pia unaweza kupata maelezo zaidi kupitia barua pepe yetu ambayo ni info@kati.ac.tz,na kwa sasa hatujaanza kutumia mtandao wa kujisajili hewani, yaani kupitia www.cas.ac.tz
Unaweza kufika chuoni kwetu kwa kupanda daladala namba 120 au 220 kutoka darajani mjini Zanzibar kuelekea bububu kidichi au unaweza kufika kwa usafiri kwa mwenyewe.
Ada kwa mwanafunzi wa cheti na stashahada zimeorodheshwa katika ukurasa wa ada
Chuo chetu kinakuhakikishia sehemu ya malazi endapo utachaguliwa kujiunga na chuo na hamna dahalia nyengine karibu na chuo, hivyo mwanafunzi anapaswa kukaa katika bweni la chuo katika kipindi chote cha masomo.
Gharama za kufanya maombi kwa mwaka wa masomo 2016/2017 ni shilling 20,000/=, lakini ada hii inakuwa inabadilika kutokana na mabadiliko ya kiuchumi
Tunatoa kozi za kilimo kwa ujumla (General Agriculture) kwa ngazi ya Astashahada (cheti) na stashahada, Uzalishaji mazao (Crop Production) kwa ngazi ya stashahada na kozi ya wanyama (Animal Health and Production).
Mahitaji madogomadogo yanapatika katika maduka yaliyomo ndani ya mazingira ya chuo ila kwa mahitaji ya vitu vya ziada unapaswa ununue mjini.